Biblia na Sayansi Inakubaliana
http://www.creationism.org/kiswahili/BibleSci_sw.htm

Wanasayansi wakati wote wamekosea katika mambo ya sayansi. Lakini sio Biblia Takatifu- ambayo imeonyesha uhalisi kisayansi. Ingawa Biblia sio maandiko ya kimsingi ya sayansi,hoja nyingi za kisayansi zimetajwa kwa mpito- na hatimaye zinapotajwa, huonyeshwa kama zilizo halali.


Wanasayansi Walikuwa Wakiamini
Lakini Sasa Sayansi Inaonyesha
Biblia Wakati Wote Husema
Eti kuna nyota kati ya elfu moja na elfu moja na mia mbili tu,ulimwenguni kote. Matrilioni juu ya matrilioni ya nyota;Haziwezi kuhesabika na binadamu. Yeremia 33:22a "Kama vile jeshi la mbinguni haliwezi kuhesabiwa..."
Dunia ni tambarare. Dunia ni mviringo. Isaya 40:22a "Yeye ndiye anayeketi juu ya duara ya Dunia..."
Mwangaza hausongi, upo pale pale. Mwangaza unaenea- na una mali asili; “wimbi la mwangaza” au fotoni. Ayubu 38:19a "Iko wapi njia ya kuyafikia makao ya nuru? ..."
Ile hali ya nadharia kuwa thabiti, nyota ziko madhubuti. Kila nyota ni ya kipekee, na nyota mbili kati ya mkusanyiko zina sharti la mvuto. Ayubu 38:31 "Jee! Waweza kuufunga mnyororo wa Kilimia, Au kuvilegeza vifungo vya orioni?"
Damu mbaya hutozwa nje ili kumfanya mtu awe vyema. Damu ni muhimu kwa maisha wakati mwingine huhitajika kuongezwa. Mambo ya Walawi 17:11a "Kwa kuwa uhai wa mwili u katika damu hiyo;..."
Hewa haina uzito, bali iko pale tu. Hewa ya oksigeni, naitrogeni na kadhalika haina uzito unaopimika. Ayubu 28:25a "Apate kuufanya upepo uzito wake;..."
Upepo huvuma upande mmoja wa dunia hadi mwingine. Hewa inayopita huenda kwa mtindo wa kuzunguka. Mhubiri 1:6b "... na upepo huyarudia mazunguko yake."
Ulimwengu umeegemea mgongoni mwa mtu fulani. Ulimwengu unaelea huru angani. Ayubu 26:7b "... Na kuutundika ulimwengu pasipo kitu."
Watu huwa wagonjwa tu; kunawa mikono sio muhimu. Magonjwa mengi huenea kutokana na mgusano. Safisha mikono na maji yanayotiririka. Mambo ya Walawi 15:13b "... naye atazifua nguo zake: naye ataoga mwili wake katika maji ya mtoni..." 
Nyota zote zinafanana. Kila moja wapo ya nyota ni ya kipekee. I Wakorintho 15:41b "...maana iko tofauti ya fahari hata ya nyota moja na nyingine in glory."
Kitu hutokana na utupu bila sababu.Utazame ulimwengu, “Mshindo mkuu” kwa mfano – puuf! Kila tendo lina kinyume kilicho sawa; hiyo ni sayansi kamili.  Chanzo huhitajika ili kutoa matokeo. Mwanzo1:1, “… Hapo mwanzo, Mungu aliziumba mbingu na nchi.”

Ingawa mwanasayansi Mgiriki Claudius Ptolemy (150 K.K) alikuwa mweledi, alifunza kimakosa kwamba dunia ilizungukwa na ulimwengu. Hapana.  Lakini unaona kuwa waliamini haya kwa miaka elfu moja.  Wanasayansi walifundisha eti ulimwengu unazunguka dunia; na wakawashawishi pia watu walio elimika, kama walivyowafanyia viongozi wa kanisa Uropa na serikali. (Biblia haifundishi haya kamwe.) yalikuwa ni mapatano ya Wanasayansi ambao walikosea na wakawashawishi wengine kuenda kinyume dhidi ya Copernicus na ya kwamba – zaidi ya miaka elfu moja – hiyo imani ya wanasayansi ilikuwa na dosari.

Galileo sio mfano wa dini dhidi ya sayansi, bali “hadithi ya Galileo” ni mfano wa mapatano ya wanasayansi waliokosea na waliwashawishi wengine walioamini hayo makosa.

Dini inaweza kuwa nzuri wakati inapo tuelekeza karibu na ukweli.

Sayansi pia inaweza kuwa nzuri wakati inapotuelekeza karibu na ukweli.

Ijapo kuwa wanasayansi ni binadamu wakati mwingine wao hukosea jinsi ilivyokuwa siku za Galileo. Kumbuka wanasayansi walikosea na walikuwa wamewashawishi wengine kuwa ulimwengu mwingine ulizunguka dunia.

Kumbuka kuwa wanasayansi walichanganya unajimu na elimu ya nyota.  Pia walichanganya sayansi ya kemia na kuwapumbaza wengi.  Kwa hivyo wakati wanasayansi wamekosea kwa muda mrefu, Biblia imebakia imara na dhabiti.  Leo hii wana mageuzi wanachanganya imani zao na za kisayansi wakati ambapo sayansi ya kweli inaonyesha ya kwamba mageuzi yanaweza kuwa sio kweli.  Lakini Biblia imetuambia ukweli kuhusu asili yetu wakati wote.  Mwanzo 1:1 “Hapo mwanzo Mungu aliziumba Mbingu na Nchi.”

Wanasayansi wa mageuzi kwa mara nyingine wamekosea kuhusu sayansi; na Biblia itaonyeshwa kuwa bado sahihi na kweli.


KUMBUKUMBU – kwa maelezo zaidi.

"Hidden Treasures in the Biblical Text" by Chuck Missler, c. 2000.  Published by Koinonia House, 120 pages.  ISBN 1-57821-127-1

"Scientific Facts in the Bible" by Ray Comfort, c.2001.  Published by Bridge-Logos Publishers, 95 pages.  ISBN 0-88270-879-1

"The Vanishing Proofs of Evolution" by Thomas F. Heinze.  Published by Chick Publications, 94 pages.  ISBN 0-758905-70-X
 

"Biblia na Sayansi Inakubaliana"
<http://www.creationism.org/kiswahili/BibleSci_sw.htm>

Hoja kuu:  Kiswahili
www.creationism.org